Thursday, March 20, 2008
Ingawa hatuna picha bado lakini taarifa ni muhimu kwenu wadau...................
Wadau wetu wote na wapenzi wa hii Blog yetu kali ya mambo ya kujiachia, tuna habari kali kwa ajli yenu wote, na habari hiyo ni kwamba katika sherehe za pasaka hapa mjini kwetu Bongo yaani Dar`es Salaam kutakuwa na shoo kali ya kukata na shoka ambayo itawahusisha wale wakali wa nyimbo za R n B waitwao Kc n Jojo kutoka Marekani au kule anakotoka Raisi Mpenzi wa midundiko kuliko hata Bwana JK mwenyewe Nikimaanisha Rais Bush. Shoo hiyo kali itafanyika katika ukumbi wa Moven Pick(Jamani tusaidiane kizungu kidogo kigumu) hapa mjini Dar es Salaam hivyo wadau wote mnaopenda mambo haya mnaalikwa! Ila kuna viingilio ambavyo ni kati ya 50,000 mpaka 80,000 hela ya madafu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment